Jumatatu, 15 Septemba 2014

IMANI YA YESU KRISTO NDANI YA MTUMISHI WA YESU KRISTO.

Matendo ya mitume 3:16[Nakwa imani katika JINA LAKE LIMEMTIA NGUVU mtu huyu mnayemwona na kumjua na imani ile ILIYOKWAKE YEYE imempatia huyu UZIMA HUU MKAMILIFU MBELE YENU NINYI NYOTE.Haya maandiko yana sehemu kuu mbili; [1]Na kwa imani katika jina lake,jina lake limemtia nguvu mtu huyu mnayemwona na kumjua; [2]..na imani ile iliyokwake yeye imempatia huyu uzima huu mkamilifu mbele yenu ninyi nyote. sehemu ya kwanza inazungumzia mtu alivyotiwa nguvu[alivyo tiwa moyo]kwa imani katika jina la Yesu,wakati sehemu ya pili inazungumzia mtu alivyoponywa[UPONYAJI MKAMILIFU] kwasababu ya imani iliyo kwake yeye[Yesu]kwa tafsiri nyepesi nikwamba kiwete; alitiwanguvu/alitiwamoyo/alipatafaraja kwasababu ya imani katika jina la Yesu na aliponywa/tatizo lake liliondolewa/aliwekwa huru kwa imani iliyo kwake Yesu,hapa tuna gundua imani za namna mbili yaaani IMANI KATIKA JINA LA YESU NA IMANI YA YESU, na utendaji wake uko tofauti,tunaona imani katika jina la Yesu imemtia moyo tu lakini imani ya Yesu imemponya ukiwete uliyokuwa unamsumbua kwa muda mrefu. Hizi namna mbili za imani nni za muhimu sana na zinategemeana sana kwani nivigumu kuwa na imani ya Yesu bila kuwa na imanni katika jina la Yesu pia huwezi kumwomba Mungu na ukapata jibu bila ya IMANI YA YESU kuwa ndani yako,imani katika jina la Yesu inakuwa kama imani ya msingi na imani ya Yesu inasimama kama imani KUU, kulingana na utandaji wake,mdo3:15[mkamuua yule mkuu wa uzima...] litaenndelea mwezi ujao...